Tanz-Hand’s – Wazo

Tanz Hand's

Tarehe 1 Augost 2009 tulifungua kitengo kipya hapa chuoni. Kiwanja chetu cha Tanz-Hand’s mahali pa kupumzika na kufurahia.
Jengo tulilochagua kwa ajili ya mradi huu liko ndani ya chuo. Tunawashukuru sana ubalozi wa Ujerumani Tanzania kwa kutuwezesha kufanyia jengo hili ukarabati. Msaada huu ulituwezesha vilevile kununua bidhaa kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya kuanza kuuza katika duka hili. Tumeanya kuuza bidhaa ambazo zinatengenezwa na walemavu tu hapa chuoni na walemavu wengine Tanzania.

Tanz-Hand’s inatoa huduma ya intaneti, kahawa freshi na tunaoka cake freshi.

Watu wamekuwa wakija tangu duka hili lifunguliwe, na linaendelea kukua kwa kasi. Tunafurahi kuwa mradi huu mpya unatusaidia katika gharama za kila siku za uendeshaji wa chuo. Hii inatusaidia kuendelea kuwapokea wanafunzi ambao familia zao haziwezi kuwalipia ada ya shule.

URRC @ Social Media

Ma mawasiliano

ELCT Usa River
Rehabilitation and Training Center
P. O. Box 47
Usa River - Tanzania

00255 / 27 255 34 27

E-Mail