Tanz-Hand’s – Bidhaa

Kabla ya Tanz-Hand kufunguliwa, wanafunzi wetu walikuwa wanatengeneza vifaa kutokana na mbao, vitambaa na matirio nyingine mbalimbali ambazo zilikuwa zinafurahiwa na wenyeji na watu toka nje.Shauku na hitaji la bidhaa zaidi lilitufanya kuzalisha kwa wingi na kuanza kuuza bidhaa hizi katika duka letu.

Kwetu sisi ni muhimu sana kuwa bidhaa tunazouza zimetengenezwa kwa mikono na zimetengenezewa hapa chuoni au katika vituo vingine venye Walemavu.  Tunalinda wazo hili kuwa bidhaa hizi zimetengenezwa kwa mikono ya Watanzania na hii inawafanya wanafunzi wetu kujivunia. Kila mmoja wa wanafunzi wetu anajua kuwa anaweza kutengeneza bidhaa nzuri na bidhaa hizi zinawafanya watu wengine wafurahie.

Tunakukaribisha kutembelea chuo chetu, Pitia dukani kwetu tufadhili kwa manunuzi yako. Tutafurahi kukuhudumia kwa kahawa na keki. Tunategemea kukuhudumia.

Hand in Hand arbeiten
Tanz Hand's Shop
 

URRC @ Social Media

Ma mawasiliano

ELCT Usa River
Rehabilitation and Training Center
P. O. Box 47
Usa River - Tanzania

00255 / 27 255 34 27

E-Mail