URRC Geografiya na maelekezo

Chuo cha Mafunzo kwa wenye Ulemavu Usa River kiko Kaskazini mwa Tanzania.  Usa River ni mji mdogo na upo kando kando ya barabara ya Arusha Moshi. Karibu na mji huu upo mlima Meru. Mpakani mwa Kenya na mlima Kilimanjaro haupo mbali.

Tanzania on the African Continent
Tanzania on the African Continent

Tanzania ilipata uhuru wake toka koloni la Waingereza mwaka 1961 na ikaungana na Zanzíbar mwaka 1964. Jina Tanzania limetokana na majina Tanganyika, Zanzíbar na Anzania.  Rais wa kwanza wa nchi hii ambaye mpaka sasa ni maarufu aliitwa Julius Kambarage Nyerere, ambaye aliiongoza nchi hii kwa siasa ya ujamaa wa Kiafrika. Siasa hii ilikufa katika karne iliyopita

Tanzania

Tanzania kwa sasa ina jumla ya watu millioni 37, kati ya hao kuna makisio kuwa asilimia 44 ni watu wenye chini ya umri wa miaka 14. Tanzania kuna zaidi ya lugha 100. Kitu kimoja ambacho kinawaunganisha Watanzania ni lugha ya taifa ambayo ni Kiswahili.  Kuna madhehebu mbalimbali: Asilimia 35 ni Waislamu, ambao wengi wanaishi Pwani na visiwani Unguja na Pemba. Asilimia 39 ni Wakristo. Pia kuna watu ambao mpaka sasa ni wapagani yaani waumini wa dini za asili.

Walutheri wapo millioni 3.5 Tanzania, na wanaongozwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Kanisa hili ni la pili kwa ukubwa kwa makanisa ya kilutheri Afrika.  KKKT ina mashule, hospitali, chekechea na vyuo vikuu. Kuanzia wakati wa ukoloni wana uhusiano kati ya kanisa la Kiinjili la Ujerumani, Kanisa la Amerika na kanisa la Scandinavia. Kuna mahusiano mengi kwa jamii na haswa misioni zina mahusiano sehemu nyingi nchini. Wanajitahidi kusaidia watu wa Tanzania katika matatizo na kuendeleza tamaduni zao kwa kushirikiana. Huu uhusiano upo, kwa mfano Usa River, inasaidiwa na Misioni ya Bavaria ( Ujerumani ya Kusini) “Eine Welt”.

Chuo chetu ni rahisi kufikika kwa barabara toka Moshi kuelekea Arusha. Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) kipo Kilometa 30 kutoka kwetu. Ramani iliyoko chini inaonyesha sehemu chuo chetu kilipo katika mji wa Usa River.

Anfahrt Zentrum

URRC @ Social Media

Ma mawasiliano

ELCT Usa River
Rehabilitation and Training Center
P. O. Box 47
Usa River - Tanzania

00255 / 27 255 34 27

E-Mail