Kwa jinsi gani misaada inasaidia

Kuwapa taswira watu wenye ulemavu ni kitu cha gharama haijalishi unaishi wapi. Lakini wakati, watu huko ujerumani na nchi nyingine za huko magharibi wanaweza kututolea misaada sisi watanzania hatuwezi. Kwa hivyo husababisha shule kama hii ya kwetu kuendeshwa kama biashara, kwa kujaribu kufanikisha kupata pesa ya matumizi. Japokuwa kila siku watu hubaki katikati ya usikivu wetu.

Ili kuwezesha kazi yetu tumekuwa tukitegemea misaada na nyongeza kutoka katika miradi yetu mbalimbali.Misaada hii husaidia kuwalipia ada wanafunzi wetu,kwa kuwa mara nyingi hawawezi kujilipia wenyewe; hapa tunapenda kukueleza ni nini unacho weza  kukamilisha na msaada wako.

  • Tshs 10.000/= hulipia kibanzi cha plastiki kutoka kwa fundi ili kusaidia watoto wenye matatizo ya miguu.Ukitibiwa ipasavyo hili tatizo hupotea kabisa baada ya miaka michache.

  • Tshs 20.000/= hulipia matumizi ya gari katika kutembea kilometa mia ambazo hutu saidia kufanya kazi  moja kwa moja huko vijijini.Kwa sababu hata leo bado tunaona wanakijiji wanaofichwa kwa hiyo inabidi watafutwe na kusaidiwa moja kwa moja katika vijiji vyao.

  • Kuishi shuleni mwezi mmoja ni gharama ya Tshs 45.000 /=. Kwa ada hii wanafunzi wetu hupata mahali pa kulala, vyakula, malezi na elimu kwa wiki nne.

  • Kwa Tshs 90.000/= tunaweza kuwasaidia mafundi viatu walio hitimu kupata vifaa muhimu na vitu vingine ili kuwawezesha kuanzisha biashara ndogo katika vijiji vyao ili waweze kuishi maisha ya kujitegemea.

  • Tshs 120.000/= hulipia gunia la maharage, ambayo ni pamoja na mahindi ni vyakula vya kila siku hapa Tanzania. Gunia moja la maharage linatosha kuwalisha wanafunzi kwa siku kumi.

  • Msaada wa Tshs 190.000/= hulipia mbao, gundi, skruu na misumari na kwa vifaa hivi tunaweza kuwafundisha wanafunzi wa useremala kwa wiki sita.

  • Baisikeli maalum zenye magurudumu matatu ambazo zinafaa kwa watu walio Walemavu ili kuwapatia usafiri. Baisikeli hizi zinaendeshwa kwa mikono na ni ukweli kwamba zina tengenezwa hapa hapa Tanzania. Baisikeli moja ni Tshs 300.000/=

  • Kwa 610.000 Tshs unaweza kumlipia Mlemavu ada yake ya mwaka mzima chuoni.

Tunakushukuru kwa msaada wako! Taarifa za akaunti yetu utazipata HAPA.

Spenden helfen!
Spenden helfen!
 

URRC @ Social Media

Ma mawasiliano

ELCT Usa River
Rehabilitation and Training Center
P. O. Box 47
Usa River - Tanzania

00255 / 27 255 34 27

E-Mail