Kazi ya kujitolea Tanzania

NGOs (Shirika lisilo la Kiserikali) inajitegemea yenyewe kimapato, misaada toka nje au ndani. Tumepata marafiki wengi duniani ambao wanatusaidia katika shughuli zetu za siku kwa siku hapa chuoni.

Kwa mfano Bwana Fritz Uhl kutoka Rothenburg o. d.Tauber amekuwa kwa muda mrefu sasa akitutumia mashine kwa ajili ya wanafunzi wetu wanaomaliza katika fani ya ushonaji nguo.  Mashine hizi zinawasaidia wanafunzi wetu waweze kuanzisha miradi yao na kujitegemea wenyewe. Jambo la muhimu ni kwamba tumekuwa na furaha kuwakaribisha madaktari na voluntia wa mradi wa Feuerkinder katika chuo chetu kuanzia mwaka 1998.

Tunashukuru sana kwa utayari wenu na msaada wenu. Tunatoa nafasi kwa baadhi ya voluntia katika chuo chetu. Kwa ajili ya kutafuta ruhusa za kukaa na kufanya kazi, visa n.k kazi hizi zinatakiwa kufuatiliwa mapema.  Kwa kuishi kwetu muda mfupi tunafurahi kukukaribisha katika nyumba yetu ya wageni.

Kwa vijana voluntia kutoka Ujerumani tunakushauri uwasiliane na missioni ya Eine Welt. Utapata habari zaidi kutoka www.missioneinewelt.de (katika kifungu kinachohusu shughuli za voluntia).

Kama unapenda kutoa msaada kwetu , tunafurahi kupokea msaada wa mawazo tunashukuru kwa kutujali.  Pia tunashukuru kwa msaada wa kifedha au vifaa. Utapata habari zaidi kuhusu jambo hili hapa.

Kwa kawaida njia nzuri ya kuwasiliana na sisi ni kwa email- unaweza kupata anwani yetu ya email hapa.

URRC @ Social Media

Ma mawasiliano

ELCT Usa River
Rehabilitation and Training Center
P. O. Box 47
Usa River - Tanzania

00255 / 27 255 34 27

E-Mail