Uzuri wa Afrika uonekanavyo katika Bahari ya Hindi

Tanzania ni mojawapo ya nchi nzuri sana Afrika ambayo ipo karibu na bahari ya hindi na ina vitu kadhaa vya asili. Ina uzuri wa asili.  Chini tumekusanya habari kuhusu utalii na safari za kitalii kwako wewe unayependa kuitembelea Tanzania.

  • Njia rahisi ya kuja Kaskazini mwa Tanzania ni kwa kutumia KLM kupitia Ámsterdam halafu KIA. Kutoka chuo chetu KIA kipo kilometa 30 tu, KIA na Usa River vimeungwa kwa barabara ya Moshi kwenda Arusha.  Kwa wageni wa chuo chetu chuo kinaandaa usafiri wa kuwafikisha chuoni ikiwa mgeni atakubali kulipa gharama za usafiri. Njia nyingine ni kusafiri na ndege ya Ethiopia kupitia Adis Ababa halafu KIA. Hii ni nafuu kwa gharama.

  • Uwezekano mwingine ni kupitia Nairobi. Hii ni rahisi, lakini inachukua muda kutoka Kenya kuja Tanzania. Na kwa kawaida utahitaji kulala Nairobi usiku mmoja. Kutoka Nairobi kuja Arusha unaweza kutumia usafiri wa basi, ambapo utatumia kama masaa saba. Ukitumia njia hii ni vizuri uwe unaijua Afrika na uwe na muda wa kutosha na hujasafiri na watoto.

View on the Kilimanjaro
View on the Kilimanjaro
The beauty of Zanzibar
The beauty of Zanzibar
 

URRC @ Social Media

Ma mawasiliano

ELCT Usa River
Rehabilitation and Training Center
P. O. Box 47
Usa River - Tanzania

00255 / 27 255 34 27

E-Mail