Nyumba yetu ya wageni inatoa huduma zifuatazo kwa urahisi kwa kulinganisha na hoteli za Arusha

Tafadhali kumbuka kuwa mapato yanayopatikana kutoka nyumba ya wageni yote yanatumika katika uendeshaji chuo. Ukiishi kwenye nyumba yetu utasaidia chuo chetu cha URRC kuendelea kuwepo.

Bei inayoonekana chini ni kwa fedha za Kitanzania Tshs / USD. Angalia hapa kulinganisha thamani ya fedha kwa wakati.


Bei ya Malazi kwa watu wanaoishi Afrika ya Mashariki Bei ya Malazi kwa Watalii au watu wanaotoka nje ya EA

chumba cha mtu mmoja chumba cha watu wawili chumba cha mtu mmoja chumba cha watu wawili
Mtu mzima: 45.000 TSh / usiku 80.000 TSh / usiku 35 USD / usiku 60 USD / usiku
Mtoto chini ya miaka 3: bure
Mtoto miaka 4 hadi 12: bei nusu

Milo
Chai asubuhi: 12.000 TSh
Chakula cha jioni: 12.000 TSh

Gharama zote za nyumba ya wageni (malazi na chakula) ni chini kulinganisha na hoteli nyingine za Arusha. Pamoja na hayo yote unapata uzuri na uchangamfu wetu bure.

Usafiri: Tunafurahi kupokea wageni wetu kutoka Kiwanja cha kimataifa cha Kilimanjaro kwa bei ya Ths. 65,000/=.  Hii ni rahisi kwa kulinganisha na bei ya kutumia teksi za pale Uwanjani.  Wageni wetu watakuwa na uhakika wa kuchukuliwa uwanjani. Unaweza kuona ramani ya nyumba yetu ya wageni hapa.

Kwa kutembelea Tanzania tunakushauri uangalie muongozo ulioandikwa na Jorg Gabriel, na kuprintiwa na the ‘Reise Know – How’ publishing house. Pia kuna miongozo mingine mizuri sana inayopatikana kwa Amazon.com (kwa mfano).

Una maswali kuhusu nyumba yetu ya wageni au utapenda kuuliza kuhusu wakati mzuri wa kusafiri? Hakuna shida!  Tutafurahi kupokea barua pepe kutoka kwa na sisi tutakujibu haraka inavyowezekana.

Tutafurahi kukukaribisha katika nyumba yetu ya wageni hapa Usa River, Tanzania karibu na mjini Arusha na Kilimanjaro.

Our guesthouse
Our guesthouse
One of the double beds in our guesthouse
One of the double beds in our guesthouse
 

URRC @ Social Media

Ma mawasiliano

ELCT Usa River
Rehabilitation and Training Center
P. O. Box 47
Usa River - Tanzania

00255 / 27 255 34 27

E-Mail