Nyumba yetu ya wageni Usa River Tanzania

Sisi kama NGO (shirika lisilo la kiserikali) tunafanya kazi zetu kutokana na misaada, pia kutokana na miradi yetu hapa chuoni na pia kwa uendeshaji wa nyumba yetu ya wageni ambayo ipo hapa Usa River Tanzania.  Japo sisi sio shirika la kitalii lakini tunathamini uzuri wa nchi hii na sana sana kwa mikoa inayotuzunguka.  Wakati wa hali ya hewa nzuri unaweza kuona mlima Meru na Kilimanjaro. Watalii wanaofahamu bei wanaweza kusafiri kwenda kwenye mbuga za wanyama, kupanda mlima Kilimanjaro na kwenda Kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro pia kusafiri kwenda mjini Arusha na Moshi kwa urahisi kwa kuwa chuo chetu kipo kando ya barabara ya Arusha – Moshi miji hii miwili inaweza kufikika kwa urahisi kwa kutumia usafiri binafsi au kwa kutumia usafiri wa barabarani (Tax, basi au Daladala).

Bett
Haus
Gästehaus

Nyumba ya wageni ipo chuoni. Imetengenezwa vizuri na ina madhari mazuri kwa kuwa inatunzwa vizuri.  Tunatoa huduma zote kuanzia malazi kwa bei nafuu. Nyumba hii inauwezo wa kulaza wageni kumi na moja. Pia kuna chumba cha sebule mahali pa kupumzikia, friji na chumba cha jiko. Pia kuna baraza mahali pa kukaa nje.

Kama utafurahiwa kuja kwetu, tutafurahi kupata maombi ya kuja kwetu.

Tafadhali angalia yafuatayo:

Google-map

URRC @ Social Media

Ma mawasiliano

ELCT Usa River
Rehabilitation and Training Center
P. O. Box 47
Usa River - Tanzania

00255 / 27 255 34 27

E-Mail