URRC - Taarifa na shughuli

Madhumuni na Historia

Chuo cha mafunzo kwa watu wenye ulemavu ni kituo cha Dayosisi ya Meru ya kanisa la Kiinjili la kiluteri Tanzania, (KKKT) Afrika ya Mashariki.

KKKT imegawanyika katika Dayosisi ishirini mojawapo ikiwa Dayosisi hii ya Meru na mkuu wa Dayosisi hii ni Askofu Paulo Akyoo. Dayosisi hii ina wastani wa wakristo 71,000. Kati ya hao kuna jumla ya watoto na vijana 43,000.

Dhumuni la kazi yetu ni kuwasaidia watu wenye ulemavu waweze kujitegemea na kuishi maisha bora zaidi.

Elimu

Kwenye chuo chetu walemavu wanapata nafasi ya kujifunza ufundi katika fani zifuatazo:

  • Ushonaji.nguo
  • Ufundi Useremala 
  • Uchomeaji vyuma
  • mwokaji (baker)

Wanafunzi wetu hupata elimu kwa miaka mitatu. Na wanafanya mitihani wa VETA.

Chuo cha walemavu ni chuo cha bweni ambacho hupokea walemavu wasichana kwa wavulana, wenye kuanzia umri wa miaka 16 hadi 25. Bila kujali kabila, rangi au dini.

Chuo hiki kilifunguliwa mwaka 1988. Hadi sasa vijana 350 wenye Ulemavu wamejifunza kwenye Chuo hiki. Chuo kina uwezo wa kupokea wanafunzi 65 tu. Chuo chetu ni cha bweni.

Huduma ya ufuatiliaji

Baada ya mafunzo na kupata matokeo mazuri wahitimu wanapewa nafasi ya kununua vifaa au vyombo vya kuanzia kazi kwa bei nafuu sana kutoka chuoni ili waweze kwenda kuanza biashara ndogo katika vijiji walivyotoka.

Matibabu kwa Mazoezi ya viungo (Physiotherapy

chuo chetu kinatoa matibabu kwa mazoezi ya viungo kwa wanafunzi wetu na kwa jamii inayozunguka chuo chetu.

Idara ya vijijini

Moja ya kazi zetu ni kuwasaidia pia wale watu wenye Ulemavu wanaoishi nje ya chuo hiki.  Idara ya vijijini inatoa huduma zifuatazo:

  • Kushauri famili
  • Kufanya mipango kwa wanaohitaji matibabau, mazoezi na elimu
  • Inatoa misaada kwa wanawake wenye watoto walemavu
  • Kuwapa walemavu misaada ya kutembelea au viungo vingine bandia (Mfano Baiskeli za walemavu, Fimbo za kutembelea nk)
  • Kuandaa na kupanga mambo ya upasuaji kwa watoto Walemavu tukishirikiana na Hospitali ya Nkoaranga upasuaji unaofanywa na madaktari toka Ujerumani.Feuerkinder

Karakana ya viungo bandia na darasa la uchomeaji vyuma

Kwenye karakana ya viungo bandia tunatengeneza kila aina ya viungo bandia. Na kwa walemavu wanaohitaji baiskeli tuna tengeneza na kurepea baiskeli hizo kwenye darasa la uchomeaji.

Nyumba ya wageni, Duka na Mradi wa shanga

Mapato mengine katika chuo chetu tunajaribu kupata kwa kuendesha miradi wa  nyumba ndogo ya wageni. Kwa yeyote anayetaka kutembelea Tanzania tunamkaribisha sana kuishi hapa kwetu. Pia tuna mradi wa shanga ambazo zinatengenezwa kwetu na kuuzwa kwenye duka letu. kama bidhaa nyingine zote zinazozalishwa chuoni.

Tunataka kuwaelewesha zaidi kuhusu kazi yetu. Kwa hiyo tumeandaa hadithi fupi kuhusu watu tunaowahuduia.

Karibuni sana!

In the carpentry
In the carpentry
In the tailory
In the tailory
In the metalworkshop
In the metalworkshop
Selling of handmade products in the Tanz-Hand´s-Shop
Selling of handmade products in the Tanz-Hand´s-Shop
In the bakery
In the bakery
The bakery-shop
The bakery-shop
Our guesthouse
Our guesthouse
 
Karibuni sana!

URRC @ Social Media

Ma mawasiliano

ELCT Usa River
Rehabilitation and Training Center
P. O. Box 47
Usa River - Tanzania

00255 / 27 255 34 27

E-Mail