Historia ya Fredi

Julai 2008 ndio tulianza kumjua Fred kwa mara ya kwanza. Anaishi na Babu yake kilometa chache kutoka chuoni kwetu UsaRiver. Mama yake alipata mimba akiwa bado mwanafunzi na baada ya kijifungua alimwacha mtoto wake hapo kijijini na hajaonekana tena kijijini hapo tokea siku hiyo.
Fred ana vidole viwili tu kwenye mikono yake yote miwili na hata miguuni ni hivyo hivyo.

Hata hivyo anauwezo wa kushika vitu na kutembea. Mpaka leo hii alisoma shule ya msingi ambayo ilikuwa kilometa sita kutoka nyumbani. Lakini kutokana na ulemavu wake ilikuwa ni vigumu kwake kwenda shule kila siku na hasa wakati wa mvua. Tulimpa viatu maalum na tukampa nafasi ya shule ya bweni kule Faraja chuo cha Madiakonia.

Picha hii anaonekana pamoja na Mchungaji Kileo, siku yake ya kwanza shuleni. Shule hii inamfaa sana Fred na mtoto huyu wa miaka 12 anaonekana kuipenda. Tunatarajia kuona maendeleo mazuri katika maisha yake ya baadae.

Fredi
 

URRC @ Social Media

Ma mawasiliano

ELCT Usa River
Rehabilitation and Training Center
P. O. Box 47
Usa River - Tanzania

00255 / 27 255 34 27

E-Mail