Usa River Rehabilitation and Training Center

Blick vom Zentrum auf den Mt. Meru

Chuo chetu ni mahali ambapo watu wenye ulemavu na wasiokuwa na ulemavu wanaishi na kufanya kazi pamoja na kwa ushirikiano “Tunaamini unaweza” ni mwongozo wautendaji na mafikira yetu. Tunaamini unaweza - Sentensi hii ina madhumuni matatu kwetu:

 1. Tunaamini unaweza - Kuishi maisha ya kujitegemea
  Kuishi kama mlemavu Tanzania, nchi maskini sana hapa duniani ni vigumu sana Hamna msaada kutoka kwenye serekali kwenye msimu wa joto walemavu huishi kwenye vumbi na kwenye msimu wa mvua huishi kwenye tope. Uwezo wa kupata elimu ni mgumu na hata wakati mwingine wanakosa elimu kabisa. Hii ni kwa sababu ya kipato kidogo cha familia yenye watoto sita au nane. Takwimu zinaonyesha kwamba mapato ya Mtanzania ni chini ya Shs.1000 kwa siku. Mpaka sasa watoto walemavu wanaonekana kama alama ya aibu na wanafichwa vijijini. Na tunaamini kwamba walemavu wengi kama wakipewa nafasi,wanauwezo wa kubadilisha maisha yao kuwa mazuri. Ndio maana tunataka kila mwanafunzi aelewe:

  Anaweza kupata maisha mazuri. Tunaamini unaweza!

 2. Tunaamini unaweza –Tajiri kutumia utajiri wako kwa ukarimu
  Familia nyingi hawana uwezo wa kulipa ada ya shule. Hata hivyo bado tunawapokea vijana wao kwenye chuo chetu. Lakini tunafanya hivyo kwa sababu kuna watu wanaojitolea kutupa msaada kwenye kazi hii. Hatuombi, lakini tunaamini kwamba ni vizuri watu matajiri wakianza kusaidia wengine kutokana na utajiri wao.  Tunahitaji kila mchango kidogo na tutashukuru sana tukiupata.  Pia, kwa wale matajiri tunasema:

  Tunaamini unaweza!

 3. Tunaamini unaweza -Na tunamtumaini Mungu kwa ajili yako
  Ni kweli kuna walemavu wengine huwa na maumivu Makali, na hutengwa na jamii, wana umaskini, hawawezi kuvumilia matatizo yao. Na sisi kama wasaidizi tunasema... kama mtu akikosa ujasiri, tunayatumainia matendo makuu ya Mungu. Kwamba anaponya. Kwamba anatupa nguvu. Kwamba anatufariji.

  Tunataka kumwambia Mungu pia.
  Tunaamini anaweza!

Elibariki Kaaya (Mchungaji) & Thomas Wollner (Shemasi)

URRC @ Social Media

Ma mawasiliano

ELCT Usa River
Rehabilitation and Training Center
P. O. Box 47
Usa River - Tanzania

00255 / 27 255 34 27

E-Mail